
KATIKA kusherehekea sikukuu ya
Krismas, Club yenye hadhi ya kimataifa katika ukanda wa Afrika Mashariki
na Kati Bilicanas, kesho inatarajiwa kuwapa burudani kabambe mashabiki
wa muziki wa disko wakiwemo watoto.
Mmoja ya
viongozi wa ukumbi huo, Hamis Omary alisema amesema leo kwamba kwamba,
kutokana na umuhimu wa sikukuu hiyo ndiyo maana wameandaa burudani
kabambe ili kutoa fursa kwa watu wa rika lote kusherehekea kwa furaha.
Alisema shamrashamra hizo
zitaanza usiku wa leo ambapo kutakuwa na usiku wa Kwaito ‘Kwaito
Special’ uliongozwa na kundi la Wakli Dancers.
Omary alisema, kesho (jumanne)
mchana kutakuwa na Watoto Shoo ambapo pamoja na muziki wa disko watoto
watakaojitokeza ukumbini hapo wataburudika na Father Krismas ambaye
atamwaga zawadi ambapo kiingilio kitakuwa sh 2,000 kwa kila motto huku
wakubwa watakaoambatana nao watalipa sh 3,000.
“Usiku wa Krismasi utakuwa na
shamrashamra nyingi ambapo watakaongia kila mmoja atapata mvinyo
mwekundu au mweupe, hii kiingilio kitakuwa sh 10,000 kwa kila
mmmoja,”alisema.
Aidha, Omary aliongeza kwamba
siku ya boxing Day ukumbi huo utaendelea kupambwa na burudani mbalimbali
ambapo kiingilio kitakuwa sh 5,000 kwa kila mmoja.
0 comments:
Post a Comment