Monday, December 31, 2012

BAADA ya danadana za muda mrefu, hatimaye Kocha Mkuu mpya wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Mfaransa Patric Lieweg, ametua nchini jana mchana huku akisema mafanikio ya kweli hayahitaji ‘kuchonga’ bali ni kazi na kwamba vitu vyake vitaonekana uwanjani kwani anajiamini juu ya uwezo wake kiufundishaji.
  Katibu wa Simba, Evodius Mtawala (kushoto) akiongozana na kocha mpya wa klabu hiyo, Patrcik Liewig baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam mchana huu.
Akizungumza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam majira ya saa 7:00 mchana, Lieweg alisema, haoni haja ya kuzungumza sana bila ya vitendo ambavyo vimemleta katika klabu ya Simba yenye makazi yake Mtaa wa Msimbazi Kariakoo.
“Mimi sihitaji kuongea sana, ila majibu ya kutoongea nina imani watu watayaona uwanjani, kwa kuwa ninajiamini nini ninakifanya,” alisema Lieweg.
Aidha, Lieweg alisema kitu muhimu ili kazi yake iweze kuonekana ni ushirikiano kutoka kwa wachezaji, benchi la ufundi na uongozi ili timu iweze kufanya vema katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Lieweg aliyechukua nafasi ya Mserbia, Milovan Cirkovic, anakabiliwa na mtihani wa kuisuka timu hiyo kuelekea raundi ya pili ya Ligi Kuu itakayoanza baadaye mwezi huu na Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo raundi ya awali itaanza mwezi ujao.
Akielezea ujio wake. Lieweg alisema ametua katika timu hiyo kwa moyo wake wote, hivyo anahitaji muda mchache tu ili aweze kukibadilisha kikosi hicho kilichomaliza mzunguko wa kwanza kikishika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na Azam FC.
  Liewing, Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Ufundi, Dani Manembe na Mtawala
Aliwashukuru wapenzi na mashabiki wa Simba, waliojitokeza uwanja wa ndege kumlaki kwa upendo wa dhati na kudai kuwa, amefarijika na jinsi ambavyo wamempokea.
Milovan alitimuliwa baada ya kwisha kwa raundi ya kwanza ya Ligi Kuu bara mwanzoni mwa Novemba, 2012 kutokana na Simba, mabingwa watetezi wa ligi hiyo, kushika nafasi ya tatu nyuma ya kinara Yanga na Azam iliyoshika nafasi ya pili.
 

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video