Sunday, December 23, 2012

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amepiga marufuku na kuagiza kuondolewa vizuizi vyote vilivyoanzishwa na Halmashauri kwenye stendi za barabara kubwa kwa ajili ya kukusanya ushuru kwani vinaleta usumbufu kwa abiria.
Kauli hiyo ilitolewa waziri huyo jijini Dar es Salaam leo, wakati alipofanya ya ziara ya kushtukiza kwenye Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi majira ya saa 11:30 alfajiri,  ili kujionea utendaji kazi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), na Kikosi cha Usalama Barabarni (Trafic), haswa katika udhibiti wa nauli holela katika kipindi hiki cha sikukuu ya Chrismas na mwaka mpya.
Alisema uwamuzi wake huo unatokana na kubaini kuwa Halmashauri hizo, zimekuwa zikiwalazimisha madereva kuingiza magari (Mabasi), kwenye vituo hivyo ambavyo siyo rasmi  kwa lengo la kujikusanyia  ushuru.
Amevitaja vituo hivyo vilivyolalamikiwa kwa usumbufu huo, kuwa ni pamoja na Mafinga, Kibaigwa, Nzega, Kibaha na vingine.
“Madereva wamekuwa wakilazimishwa kuingia katika stendi hizi hata kama hawana abiria wakushuka amakupakia, kitendo ambacho kinawapotezea abiria muda wao wakufika kule wanakokwenda bila sababu za msingi”alisema Dk Mwakyembe.
Alisema utaratibu huo haukubaliki, endapo ukiachwa uendelee hivyo iko siku watazuka watu watafikia hatua ya kuanzisha vizuizi kama hivyo majumbani mwao lengo likiwa ni kuibia wananchi.
Dk Mwakyembe amezitaka Halmashauri hizo kuacha utaratibu huo na baadala yake watafute vyanzo vingine vya ukusanyaji mapato.
 

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video