Monday, January 30, 2017



Kagera Sugar wamemuenzi vyema Golikipa wao, David Abdallah Burhan ambaye amefariki Dunia Usiku wa Kuamkia leo  baada ya kuichapa 2-1 Mtibwa Sugar kwenye mechi ya Ligi kuu soka Tanzania Bara iliyochezwa leo Jioni Uwanja wa Kaitaba, Mkoani Kagera.
Mabao ya Kagera Sugar  kwenye 'Dabi' hiyo ya Sukari yalifungwa na Mbaraka Yusuph na Ibrahim Twaha, wakati la kufutia machozi kwa Mtibwa Sugar liliwekwa wavuni na Stamil Mbonde.
Mbaraka sasa amefikisha mabao 9 msimu huu wa Ligi kuu sawa na Amissi Tambwe wa Yanga, Shiza Kichuya wa Simba na Simon Msuva wa Yanga.
 Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar wamejikita nafasi ya tatu wakifikisha pointi 37 baada ya kucheza mechi 21, wakati Mtibwa Sugar wanaendelea kuwepo nafasi ya tano kwa pointi zao 31.
Mchezo mwingine ulichezwa Uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga ambapo wenyeji JKT Ruvu walitoka suluhu (0-0) dhidi ya Stand United.
JKT Ruvu wanaendelea kuburuza mkia wakiwa na pointi 16, pointi tatu nyuma ya Ndanda wanaoshika nafasi ya 15 wakiwa na alama 19.

FT: Kagera Sugar 2-1 Mtibwa Sugar
FT:JKT Ruvu Stars 0-0 Stand United
 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video