Leo Manchester United wanaikaribisha Arsenal kwenye Dimba la Old Trafford, mchezo wa Ligi Kuu ya England utakaofanyika saa 9.30 kwa saa za hapa nyumbani.
Rekodi muhimu kuelekea mchezo huu
1. Manchester United wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya mechi kumi za hivi karibuni walizocheza dhidi ya Arsenal. Hiyo ilikuwa mwezi October 2015 ambapo United walipoteza 3-0 kwenye uwanja wa Emirate.
2. Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho hajawai kupoteza mchezo dhidi ya Arsenal kwenye mechi za ligi kuu nchini England. Ameshinda mechi tano na kutoka sare mara sita.
3. Mechi ya Manchester United dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Old Trafford imetoa penati kumi. Kati ya penati hizo sita zimeshindwa kuingia nyavuni.
4. Mshambuliaji wa Man United, Wyne Rooney ameifunga Arsenal mara kumi na nne kwenye mechi zote za mashindano.
0 comments:
Post a Comment