Thomas Muller ndiye alikuwa nyota wa mchezo, Ujerumani ikiichapa 3-0 Norway na kuwafanya waanze vizuri harakati za kuelekea kutetea taji lao la kombe la Dunia mwaka 2018 Nchini Urusi.

Mechi hiyo ya kundi C ya kuwania kucheza World Cup 2018 ilichezwa uwanja wa Ullevaal Stadion Mjini Oslo.

Mshambuliaji huyo wa Bayern Munich, alifunga mabao mawili na kutoa pasi murua ya mwisho kwa bao la Joshua Kimmich ambaye alicheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wakubwa.


0 comments:
Post a Comment