Friday, September 2, 2016

Mchezaji Bastian Schweinsteiger amejumuishwa kwenye kikosi cha mwisho cha klabu ya Manchester United ambacho kitashiriki ligi kuu ya Uingereza chenye wachezaji 25.

Bastian amekuwa katika msuguano na kocha wake Jose Mourinho ambaye tangu anafika labuni hapo alionekana kutokumkubali na kuwa hakuwa akiendana na ahitaji yake ndani yaklabu hiyo.

Mourinho alienda mbali zaidi na kumruhusu mchezaji huyo kuweza kuondoka katika klabu hiyo ya jijini Manchester. Hata hivyo Bastian aligoma kwa maana ya kuwa asingeweza kuchezea klabu yoyote tofauti na Manchester kwa Ulaya. Akaweka bayana kuwa baada ya Bayern Munich, klabu ya mwisho ilikuwa Manchester United.

Wiki iliyopita Jose Mourinho alisema kuwa “ni vigumu sana kwa Bastian kucheza chini ya yangu na kwenye kikosi changu, lakini haina maana kuwa haiwezekani.”

Katika siku za mwanzo za maisha ya Mourinho pale Carrington, Bastian Schweinsteiger alitakiwa kufanya mazoezi na timu ya wachezaji wa akiba pamoja na vijana. Jambo hili lilizua maswali pamoja na kupelekea Mourinho kukosolewa kwa kiasi kikubwa hasa na wadau wa soka la Ujerumani.

Siku ya juzi, Bastian alicheza mchezo wkae wa mwisho na kugawa kwa hisia kali na wachezaji na mashabiki wa timu ya Taifa ya Ujerumani. Katika mchezo huo dhidi ya Finland uliofanyika Monchengledbach, Bastian alishindwa kujizuia kutokwa na machozi huku akishuhudia uwanja mzima ukipiga makofi kwake wakati anafanyiwa mabadiliko.

Bastian amechezea timu ya taifa michezo 121 huku pia akiwa amefunga mabao 24. Mchezo wake wa kwanza na timu hiyo ulikuwa miaka 12 iliyopita, mwaka 2004.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video