
Liverpool wameendeleza rekodi yao nzuri kwenye michezo ya hivi karibuni baada ya kuwapa kipigo kizito cha mabao 3-0 Derby wanaocheza Ligi ya Daraja la Kwanza na kufuzu raundi ya nne ya Michuano ya EFL Cup.
Ragnar Klavan alianza kuipa Liverpool goli la kwanza baada ya kuunganisha mpira safi wa kona uliochongwa na Philippe Coutinho.
Philippe Coutinho aliipa Liverpool goli la pili baada ya kugongeana pasi safi na Roberto Firmino, kabla ya Divock Origi kumalizia goli la tatu.
Derby walijitutumua muda wote wa mchezo na kufanikiwa kupiga mashuti mawili ambayo hata hivyo yaliishia mikononi mwa kipa aliyecheza kwa mara yake ya kwanza Loris Karius.
Hii ni mechi ya nne mfululizo Liverpool wakishinda mabao matatu na kuendelea na kufanikiwa kufunga mabao 19 katika jumla ya michezo saba.
0 comments:
Post a Comment