Hatimaye baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu, Paul Pogba ametua jijini Manchester kupima afya kwa ajili ya kusajiliwa na Manchester United kwa dau linalokwenda kuvunja rekodi ya dunia la Euro milioni 110 akitokea klabu ya Juventus ya Italia.
Kurejea kwa Mfaransa huyo Old Trafford imekuwa stori kubwa ya usajili majira haya ya kiangazi, lakini sasa amewasili na alipotua ameendeshwa akiwa kwenye gari kuelekea Aon Training Complex kuchukua vipimo vya Afya.

Pogba tayari yupo Mjini Manchester

Pogba akiendeshwa kuelekea kupima afya mchana wa leo

Pogba alipigwa picha akiwasili Manchester

Mfaransa huyo ametua na ndege akitokea New York
0 comments:
Post a Comment