Mabingwa wa soka nchini na wawakilishi pekee katika Michuano ya Afrika Yanga SC, leo jioni saa 12:00 (kwa saa za hapa Tanzania) watakuwa Uwanja wa Sekondi Sports au Essipong mjini Sekondi-Takoradi, Ghana kuwakabili Medeama SC kwenye mchezo wa raundi ya pili wa makundi katika Kombe la Shirikisho Afrika.
Katika mchezo wa awali uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga walilazimishwa suluhu ya goli 1-1.
Yanga itamkosa beki wake Mtogo Vicent Bossou ambaye anatumikia adhabu ya kadi ambapo Nadir Haroub anatarajiwa kuziba pengo hilo. Deus Kaseke na Geofrey Mwashiuya pia hawatakuwepo kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Yanga wanatatakiwa kufanya kila wawezalo kushinda mchezo wa leo ili kufufua matumaini ya kusonga mbele. Matokeo mengine kinyume na hayo yatakuwa yameinyima nafsi Yanga ya kujiandalia mazingira ya kufuzu hatua ya nusu fainali.
Mchezo huo utarushwa na kituo cha runinga Super Sport (SS9).
0 comments:
Post a Comment