
WINGA wa Yanga, Simon Msuva amefichua kuwa mafanikio yako katika msimu uliomalizika yalikolezwa na kocha wao msaidizi,Juma Mwambusi.
Yanga ilifanikiwa kutetea taji la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu pamoja na kutwaa Kombe la Shirikisho(FA Cup).
Akizungumza na BINGWA juzi, Msuva alisema anaamini mafanikio yao hayo yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na kocha huyo wa zamani wa Mbeya City ya jijini Mbeya.
Msuva alimsifu kocha wake huyo kwa kusema alitimiza majukumu yake kwa ufasaha kama msaidizi wa kocha wao mkuu, Hans van de Pluijm.
Msuva alimwelezea Mwambusi kama kocha aliyewahimiza wachezaji wake umuhimu wa nidhamu, kujituma na kucheza soka ya kushambulia hatua iliyowawezesha kutimiza matarajio yao.
“Ukichanganya falsafa ya makocha wote ndiyo unaipata Yanga ya sasa, naamini uwepo wao utaendelea kuifanya Yanga ifanye vizuri ndani na nje,” alisema Msuva.
Mwambusi alijiunga na Yanga msimu wa 2013/14 wa Ligi Kuu Bara, akitokea kuwa kocha mkuu wa Mbeya City baada ya aliyekuwa kocha msaidizi wa Yanga,Charles Mkwassa kuteuliwa kuifundisha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
0 comments:
Post a Comment