Ivo alisema: “Ni kipa asiyependa kulewa sifa, anajua kazi iliyompeleka Azam, anajifunza wakati wote, haoni kwamba amefika mwisho mchezaji wa staili hiyo milango ya kupenya umbali mrefu ipo wazi kwake kwani amekuwa tofauti kabisa na baadhi yao wanalewa sifa mapema,”
KIPA mkongwe Ivo Mapunda, amemwangalia Aishi Manula anayecheza naye Azam na kutamka kwamba kipa huyo ana uwezo wa kufika mbali zaidi kwa sababu ana malengo na hupenda kujifunza na kukubali makosa yake.
Ivo alisema: “Ni kipa asiyependa kulewa sifa, anajua kazi iliyompeleka Azam, anajifunza wakati wote, haoni kwamba amefika mwisho mchezaji wa staili hiyo milango ya kupenya umbali mrefu ipo wazi kwake kwani amekuwa tofauti kabisa na baadhi yao wanalewa sifa mapema,”
Ivo alisema suala la Manula kuwepo ndani ya kikosi cha Azam anaamini atakuwa msaada mkubwa kwenye Ligi Kuu na michuano mingine ikiwemo Kombe la FA lililo chini ya TFF pamoja na michuano ya kimataiafa ya Kombe la Shirikisho ambayo timu hiyo inashiriki na sasa inajiandaa kuivaa Esperance ya Tunisia wikiendi ijayo.
“Kadri anavyopata mechi nyingi, anajifunza mambo mengi. Kwa kuwa ana anapenda kujifunza mazuri atakuwa kipa hatari VPL, kikubwa aendeleze juhudi bila kuchoka ili afikie mafanikio yake,” alisema.
Manula aliwahi kukaririwa na Mwanaspoti akisema; “Uzoefu wa kipa Mapunda, umekuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi cha Azam, kwani amekuwa akitusaidia kutufundisha mengi,” alisema.
Manula alisema anatumia muda wake mwingi kujifunza na makipa wa timu yao ya vijana hilo linamfanya azidi kujiimalisha na kutambua ni wapi anapoweza kuongeza juhudi zaidi kwa ajili ya ufanisi zaidi.
0 comments:
Post a Comment