Sunday, March 20, 2016

Haruna Niyonzima akipampa mkono nahodha wa APR, Jean Claude Iranzi kwenye mechi ya kwanza jijini APR. 

Yanga watamkosa kiungo wao mchezeshaji Haruna Niyonzima kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utaochezwa tarehe 9 mwezi ujao jijini Dar.
Kiungo huyo raia wa Rwanda, ataukosa mchezo huo wa wa raundi ya mwisho ya kufuzu hatua Nane Bora kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano katika mechi mbili dhidi ya APR ambapo Yanga walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 3-2.
Katika mchezo wa awali jijini Kigali, Niyonzima aliyekuwa nahodha alipewa kadi ya njano na hivyo hivyo katika mchezo wa marudiano jijini Dar alioneshwa kadi ya njano mapema kipindi cha kwanza.
Wachezaji wengine wa Yanga, Donald Ngoma na Amissi Tambwe itabidi waje kwa tahadhari kwenye mechi ijayo baada ya kuoneshwa kadi za njano hio jana.
Credit:Soka 360

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video