
Everton walizifungua nyavu za Chelsea zikiwa zimebaki dakika 15 kabla ya mchezo wa robo fainali ya FA Cup kumalizika na huyo hakua mwingine bali ni Romelu Lukaku.
Striker huyo wa zamani wa The Blues alifunga bao lake la kwanza dhidi ya waajiri wake wa zamani kuiweka Everton mbele.
Goli hilo ambalo linafananishwa na magoli ya Ryan Giggs na Ricky Vill kwenye michuano ya FA, Lukaku aliwaacha wachezaji wanne wa Chelsea kabla hajapachika mpira kambani.
Mchezo huo ulimalizika kwa Chelsea kuchapwa bao 2-0 bao la pili likifungwa pia na Lukaku.

0 comments:
Post a Comment