
Baba wa Eden Hazard amedai kwamba Chelsea wanamlazimisha mwanaye kucheza licha ya kusumbuliwa na majeraha, na kusisitiza kwamba hakukuwa na ulazima wa kucheza katika mchezo wa PSG isipokuwa kutokana na umuhimu wake katika kikosi hicho.
Hazard alizomewa na mashabiki wa Chelsea katika mchezo dhidi ya PSG wakati akifanyiwa mabadiliko na kuingia Oscar.
Akiongea na gazeti la Le Soir la nchini Ubelgiji alisema: "Kiwango kinachooneshwa na Eden kwa sasa ni kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara, maumivu ya nyonga, ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa takribani miezi mtatu au minne.
"Sio kwamba ana majeraha makubwa lakini tatizo ni maumivu, hali hiyo ndiyo ilisababisha kuomba kutolewa katika mchezo dhidi ya PSG.
"Badala ya kumpa muda wa kupumzika ili apone vizuri, wanataka kumchezesha muda wote, sababu kubwa ikiwa ni kwamba huu ulikuwa mchezo uliobeba umuhimu mkubwa.
"Unadhani ni mchezaji gani katika mchezo wa soka ambaye hajawahi kupitia kipindi kigumu katika maisha yake ya soka? Tangu aanze kucheza soka katika kipindi chote cha maisha yake ya soka, hii ni mara yake ya kwanza. Sio mashine huyu ni binadamu."
0 comments:
Post a Comment