
Mshambulizi wa Manchester City Aguero 'Kun' amesema ataondoka Ligi Kuu Uingereza pale mkataba wake na klabu ya Manchester City utakapomalizika.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu wa 2018-19.
Akiwa na klabu ya Manchester City, Aguero ameifungia magoli 128 tangu alipowasili kutoka klabu ya Atletico Madrid mwaka 2011 kwa uhamisho uliogharimu ada ya paundi milioni 38 2011, akiwa ameshinda makombe mawili ya Ligi Kuu klabuni hapo.
Aguero, 27, alisema hayo wakati akiongea kwenye kituo kikomja cha radio nchini Argentina. "Hilo lipo wazi kwamba anatarajia kurdi kwenye klabu yake ya utotoni ya Independiente na kustaafia pale".
"Hapa klabuni wanjua fika ninachotaka kufanya, wanafahamu ninataka kurejea nchini kwangu (Argentina)," aliongeza.
"Familia yangu inafahamu kwamba nitarejea mkataba wangu ukimalizika hapa Manchester City mwaka 2018."
0 comments:
Post a Comment