Saturday, February 13, 2016

Hamisi Kiiza akishangilia goli lake la kwanza dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga

Mabao mawili ya Hamisi Kiiza yanaipandisha Simba kileleni mwa ligi kwa mara ya kwanza baada ya kusubiri kwa misimu mitatu bila kukaa kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara na kuacha ligi hiyo ikitawaliwa na mahasimu wao Yanga, Azam na Mtibwa Sugar ambao wamekuwa wakipokezana kuongoza ligi hiyo.
Kwa mara ya mwisho Simba iliongoza ligi mwanzoni mwa msimu wa 2013-14 wakati huo Simba ikiwa chini ya kocha Abdalah Kibadeni aliyekuwa akisaidiwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kuiongoza Simba kushinda michezo yake mitano ya mwanzo.
Ibrahim Ajib (kushoto) akipambana na beki wa Stand United

Bao la kwanza la Hamisi Kiiza lilitokana na krosi ya Mwinyi Kazimoto ambayo ilimkuta Ibrahim Ajib ambayea lipiga mpira uliomgonga beki wa Stand United na kumkuta Kiiza aliyeachia shuti kali lililomshinda golikipa wa Stand Frank Muwonge.
Goli hilo liipa Simba nafasi ya kuongoza 1-0 mpaka dakika za kipindi cha kwanza kinamalizika huku Stand wakiwa hoi.
Nahodha wa Stand United Jacob Masawe (kulia) akimzuia Ajib

Kipindi cha pili Simba walipata bao la pili dakika ya 48 ikiwa ni dakika tatu tu tangu kipindi cha pili kuanza baada ya Hassan Kessy kumtoka kutbeki wa kushoto wa Stand United na kuambaa na mpira kisha kutia krosi ambayo ilikwamishwa moja kwa moja wavuni na Hamisi Kiiza ‘Diego’.
Pastory Athanas aliipa Stand United bao la kufutia machozi dakika ya 89 baada ya walinzi wa Simba kujichanganya na kushindwa kuokoa mpira langoni mwao.Mwinyi Kazimoto (katikati) akisaidiwa kutoka nje na madaktari baada ya kuumia uwanjani

Mwelekeo wa ligi
Simba wamerejea kwenye mbio za ubingwa wakitokea nafasi ya nne nyuma ya Mtibwa Sugar na kukwea mpaka nafasi ya kwanza huku wakiwa mbele kwa mchezo mmoja dhidi ya Yanga lakini wakiwa mbele ya Azam kwa michezo mitatu (3). Simba imecheza michezo 19, Yanga 18 wakati Azam ambao watacheza kesho wakiwa wameshacheza mechi 16.

Rekodi ya Mayanja tangu atue Simba
Jackson Mayanja aliichukua Simba chini ya Dylan Kerr ikiwa nafasi ya tatu ameingoza kwenye michezo sita ya ligi kuu ya Vodacom na kufanikiwa kushinda michezo yote na kukusanya jumla ya pointi 18 huku akiwa ameingoza pia katika ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Burkina Faso kwenye mchezo wa FA Cup.

Kuelekea Kariakoo Derby (Yanga vs Simba)
February 20 Simba wataingia kwenye mchezo dhidi ya Yanga wakiwa na morali ya juu baada ya kushinda michezo yao sita kabla ya pambano hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wao huku wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 2-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza.
Credit:Shaffih Dauda

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video