Baada ya Real Madrid kupokea kipigo cha 1-0 kutoka mahasimu wao Atletico Madrid nyumbani kwao Santiago Bernabeu juzi usiku – FC Barcelona jana waliwakaribisha Sevilla Nou Camp katika kujaribu kuongeza utofauti wa pointi dhidi ya wapinzani wao.


Rekodi ya FC Barcelona ilianzia mwanzoni mwa msimu huu mara baada ya kufungwa na Sevilla mnamo October 2015, na tangu mechi hiyo Barca wamecheza mechi 34 za mashindano yote bila kupoteza na kuifikia rekodi ya Real Madrid ya msimu wa 1988-89.
Kikosi cha Real Madrid kilichokuwa chini ya kocha Leo Beenhakker na nyota mastaa kama Butragueño, Hugo Sánchez, Michel na Schuster ndio ilikuwa timu ya mwisho Spain kuweka rekodi hiyo. Kikosi hiki cha Madrid kilifanikiwa kushinda mataji manne mfululizo ya la Liga.


Barcelona hii ya sasa inayoongozwa na MSN ya Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar, chini ya kocha Luis Enrique imeshafanikiwa kutwaa makombe ya La Liga, Champions League na Copa del Rey msimu uliopita na wakaja kuongeza makombe mengine mawili mwanzoni mwa msimu huu.
0 comments:
Post a Comment