Manchester City leo wapo nyumbani wakiwakaribisha vinara wa Ligi Leicester City, ikiwa ni fursa pekee kwao kwenda kileleni endapo wataibuka na ushindi katika mchezo huo. Wakati huohuo, ni nafasi kwa Leicester pia kuongeza pengo la pointi na kufikia 6 endapo wataibuka na ushindi na kuongeza uwezekana wa kuchua ndoo.
Mchezo huo utapigwa majira ya saa 9;45 Alasiri kwa saa za Afrika Mashariki, Man City wapo katika nafasi ya pili mbele ya Arsenal kwa pengo la pointi mbili na nyuma ya Leicester kwa pointi tatu na endapo watapata ushindi siku ya leo basi watakwea moja kwa moja kileleni kutokana na kuwa na tofauti nzuri ya magoli ya kufunga na kufungwa, City wakiwa na magoli 23 huku Leicester wakiwa na magoli 18 hivyo kuwa na tofauti ya magoli 5.
Licha ya kutokuwepo kwa Kevin de Bruyne kutokana na majeraha, lakini uwepo wa Sergio Aguero 'Kun' ambaye yupo katika kiwango bora kabisa ni silaha kuwa kwa Man City katika mchezo wa leo akiwa amefunga goli lake la 12 katika michezo 10 ya mwisho.
Mustakabali wa kocha Manuel Pellegrini tayari umeshaamuliwa lakini bado ana kazi kubwa ya kufanya mpaka mwisho wa msimu na kuchukua kombe kwa mara yake ya pili ili kuondoka kwa heshima klabuni hapo na kumkabishi mikoba Pep Guardiola. Man City wamefanikiwa kushinda michezo nane kati ya 12 ya mwisho waliyocheza katika dimba lao la nyumbani la Etihad hivyo kuwapa matumaini ya kuibuka na ushindi katika siku ya leo.
Wakati huohuo, Leicester wameruka viunzi vingi sana msimu huu, wakiwa kileleni licha ya watu wengi kutowapa nafasi ya kutwaa ubingwa. Ushindi kwao utakiwa ni kitu muhimu katika kuongeza morali yao hasa nyakati hizi za kuelekea katika muda wa lala salama, wakikabiliwa na mchezo mwingine mgumu dhidi ya Arsenal wiki ijao.
Vijana hao wa Claudio Ranieri wanaingia katika mchezo huu wakiwa tayari wamewanyoa Majogoo wa jiji la Liverpool katikati mwa wiki iliyopita lakini wakiwa wanajua fika jinsi kibarua cha leo kilivyo kigumu kunako dimba la Etihad, Hata hivyo kurudi kwa Jamie Vardy katika ubora wake wa kufunga ni kitu kinachowapa nguvu kubwa vijana hao wa Ranieri.
Makocha wanasemaje?
Manuel Pellegrini: "Si kana kwamba ndio mchezo wa kuamua bingwa msimu huu. Ligi hii haiishii hapa. Bado kuna michezo mingi sana ya kuhakikisha tunakuwa mabingwa. Ni muhimu sana kila mmoja kufahamu kwamba nilikuwa najua kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Hii ni mara yangu ya mwisho kuongelea hili jambi tena. Tunatakiwa kuangalia tunamaliza vipi michezo iliyobaki. Siongelei mustakabali wangu hapa, wewe niulize kuhusu timu yangu na michezo inayofuata, hapo nitakujibu."
Claudio Ranieri: "Hata kama tukishinda, lakini piatunaweza kupoteza dhidi ya Arsenal. Ni vigumu sana kusema hili (kwamba Leicester anaweza kuwa bingwa). Tunataka mashabiki wetu kuwa na matumaini lakini tunajua fika kwamba ni mchezo mgumu na kuanzia sasa kutakuwa na michezo migumu mno. Tunakiwa kuendelea kama hivi. Mara zote nawaambia wachezaji wangu, tulimaliza raundi ya kwanza tukiwa na alama 39, sasa raundi ya pili nataka tumalize tukiwa na alama 40, moja zaidi. Tunatakiwa kuchukua angala alama mbili kwa kila mchezo mpaka mwisho wa msimu tuwe na pointi 79. Sasa sijui kama zitatosha kutufanya tuwe mabingwa, lakini nataka kuboresha hili. Kma hatutakuwa bora, bado tumekuwa na msimu mzuri hata ikitokea tumeshuka. Naamini inaweza kutokea tukapoteza mchezo wowote, lakini muhimu ni kuhakikisha kila mchezo tunacheza kwa nguvu zetu zote."
Utabiri wa vikosi vitakavyokuwa
Manchester City
Hart; Sagna, Otamendi, Demichelis, Kolarov; Fernandinho, Fernando; Silva, Toure, Sterling; Aguero
Leicester City
Schmeichel; Simpson, Morgan, Huth, Fuchs; Albrighton, Drinkwater, Kante, Mahrez;Vardy, Okazaki
0 comments:
Post a Comment