Habari kuhusiana na Jose Mourinho kujiunga na Manchester United zimeibuka tena wiki hii ambapo baadhi ya vyombo vya habari vya Ureno na Hispania vimekuwa vikikaririwa vikiripoti kwamba Mourinho tayari amesaini mkataba wa awali kwa ajili ya kutua Old Trafford majira ya kiangazi ya msimu huu.
Tayari gazeti la jijini Madrid (Marca) limeripoti hadi tarehe ambayo Mreno huyo atatua kwenye kikosi cha Man United ambapo inataarifiwa kwamba atachukua mikoba ya kukinoa kikosi hicho itakapofika July 1 mwaka huu.
Japokuwa Louis van Gaal anapita kwenye changamoto nyingi za kupanda na kushuka bado hisia za kwamba hatoweza kumaliza mkataba wake wa miaka mitatu zinazidi kupamba moto, anaweza akajiuzulu mwenyewe au kupigwa chini wakati wa majira ya joto.
Kuondoka kwa Van Gaal kutaiacha ajira ya ukocha wa United wazi na Mourinho ndiye kocha anayepewa nafasi kubwa kuchukua nafasi hiyo ifakapo tarehe 1 mwezi July wakati wa pre-season.
Akiwa ametupiwa virago vyake na Chelsea mwezi December mwaka jana, kocha huyo wa kireno anatazamiwa kuwa kocha mpya kwenye dimba la Old Trafford.
Marca wanazidi kusema kwamba, uongozi wa United uko tayari kumtimua Van Gaal na kumuachia timu Ryan Giggs kwenye kipindi hiki endapo matokeo ya timu yao yataendelea kuwa mabaya lakini Mourinho hatapewa mikoba hiyo kwa sasa hadi mwisho wa msimu huu.
0 comments:
Post a Comment