Mlinzi hodari wa zamani wa Arsenal Martin Keown anasema anataraji kwenda kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa White Hart Lane, maskani kwa Tottenham Hotspurs tangu alipoingia wakati akicheza Arsenal iliyomaliza ligi bila ya kufungwa mwaka 2004, kushuhudia mchezo kati ya Spurs na Watford.
Lengo kubwa la kwenda huko ni kwa ajili ya kushuhudia namna ambavyo walinzi wa Spurs wanavyofanya timu hiyo ipate matokeo mazuri.
Keown anasema kuwa wakati akiwa mchezaji, mara nyingi alitumia wakati wake kuwaangalia mabeki mbalimbali na kujifunza kitu kimoja ama viwili.

Wachezaji wa Spurs wakishangilia moja ya magoli yao

Kocha wa Spurs Mauricio Pochettino amepandikiza mchezo wa aina yake kunako klabu ya hiyo.
Keown anasema kwamba imekuwa ni jambo la kuvutia kuwaangalia namna Spurs wanavyocheza msimu huu. Wanafanya mashambulizi ya haraka na kuwapanikisha mabeki wa timu pinzani na kuwafanya wajichanganye hivyo kupata magoli kirahisi.
Anasema kwamba, timu pinzania itaishia kupiga mira mirefu na kuishia kwa mabeki Toby Alderweireld na Jan Vertonghen, ambao ni mahiri sana kwa mipira ya aina hiyo hivyo kuwapa wakati mgumu wapainzani.

Toby Alderweireld (wa pili kulia) amekuwa ni sehemu muhimu ya safu ya ulinzii ya Spurs msimu huu

Kevin Wimmer (kulia) na Dele Alli pia ni nguzo muhimu kwa Spurs
Anasema kwamba ni kitu cha kuvutia kwamba Spurs inashika nafasi ya pili miongoni mwa timu zilizofanya faulo nyingi kunako ligi kuu England msimu huu na nyingi zikitokea upande wa timu pinzani.
Anaendelea kusema kwamba hii inatokana na kocha wao kuwafundisha wachezaji wake kuwa na njaa ya kuwa na mpira muda mwingi wa mchezo ili kuzuia hatari zinazoweza kwenda langoni mwao.

Keown anasema kuwa hii ndiyo ilikuwa siri ya mafanikio kwa Arsenal ya mwaka 2004 na kufikia hatua ya kuchukua ubingwa bila ya kufungwa.
0 comments:
Post a Comment