Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto) akithibitisha serikali kumzawadia Samatta fedha na kiwanja maeneo ya Kigamboni
Kwa kuthamini tuzo aliyotwaa nahodha wa timu taifa ya Tanzania Mbwana Samatta, Selikali kupitia wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imemkabidhi nyota huyo kiwanja eneo la Kigamboni ikiwa ni sehemu ya kujali na kuthamini heshima ambayo Samatta ameiletea Tanzania ya kuwa mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani (ligi za Afrika).
Samatta amepewa kiwanja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi kwenye sherehe maalum ya kumpongeza Mbwana Samatta kwa kutwaa tuzo hiyo iliyoipa heshima kubwa Tanzania. Tuzo hizo zimefanyika usiku wa Jumanne January 12, 2016.

Thomas Ulimwengu alikuwepo pia kumsapoti Samatta ambaye wamecheza pamoja TP Mazembe kwa muda mrefu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akithibitisha serikali kumzawadia Samatta fedha na kiwanja maeneo ya Kigamboni
Samatta (katikati), Waziri mwenye dhamana ya michezo Nape Nnauye (kushoto) na waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe (kushoto) na mwandishi maarufu wa habari za michezo Saleh Ally
Mbwana Samatta akimkabidhi zawadi ya jezi Waziri wa Ardhi, Nyma na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi
Picha zote kwa hisani ya Vodacom
0 comments:
Post a Comment