Marco Verratti anaamini kwamba Paris Saint-Germain hawana tatizo juu ya kumuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic.
Mkataba wa Zlatan unaisha mwishoni mwa msimu huu, huku PSG mpaka sasa wakiwa hawajafanya naye mazungumzo yoyote juu ya mkataba wake
"Kama mimi ndiyo ningekuwa rais wa PSG nisingepatwa na kigugumizi juu ya kumuongezea mkataba,"alisema Verratti
"Namjua Ibra vizuri sana, namwona kila siku mazoezini, na kwangu, bado namwona kwenye ubora wake"
Verratti pia aliongeza kwa upande wake anajisikia vizuri sana kubaki PSG na hana mpango wowote wa kuondoka hivi karibuni.
"Sifahamu ni lini nitaongeza mkataba wa kuendelea kubaki hapa. Nataka kufanya hivyo lakini muulize rais wangu."
0 comments:
Post a Comment