Monday, December 21, 2015

Mesut Ozil ameahidi kuwa kamwe hutomwona akijiangusha ama akijaribu kumdanganya mwamuzi pindi awapo uwanjani
Kiungo huyo mchezeshaji, ambaye yuko kwenye kiwango cha juu hivi sasa akielekea kuvunja rekodi ya gwiji wa klabu hiyo Thierry Henry kwa kutoa pasi za magoli kwa msimu, tayari ameshatoa pasi za magoli 13 mpaka sasa.
Huku baadhi ya wanasoka wakubwa ulimwenguni wakisifika kwa vitendo vya kujiangusha, na Cristiaono Ronaldo akiwa miongoni mwao, Ozil amekuwa akisifika sana kwa aina yake ya mchezo kwa kutojiangusha hovyo lakini vilevile kutokuwa mchoyo awapo uwanjani
Hivyo basi, Ozil amefichua siri ya kuwa hivyo na kusema kwamba hali hiyo imetokana na mazoea aliyojijenge awakati akiwa katika umri mdogo kutokana na kucheza katika viwanja ambavyo haikuwa rahisi kujiangusha kwa sababu ya ubora mdogo wa viwanja hivyo.
 “Inanifanya nijisikie vizuri sana kusikia hizo taarifa. Hivyo ndivyo nilivyo,”alisema Ozil wakati akiongea na The Times.
 “Nimekuwa katika hali hiyo, siku zote nimekuwa mkweli uwanjani.  Sitabadilika. Sijiangushi. Kamwe siwezi kufanya hivyo. Wakati naanza kucheza soka nilikuwa nikicheza katika uwanja mgumu sana, na nisingeweza kujiangusha hovyo kutokana na kuhofia kuumiza miguu yangu. Katika baadhi ya maeneo kulikuwa na mawe.”
“Ndiyo maana hatukuwa tukijiangusha hovyo, kamwe hatukujifunza kujiangusha. Hatukuwa na uwanja ambao ungesapoti sisi kujiangusha. Na hata kwenye viwanja vyenye nyasi bora pia najitahidi sana kutojiangusha.”

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video