Sunday, December 20, 2015

Thomas Muller amesema kuwa wachezaji wa Bayern Munich hawana wasiwasi wowote juu ya hali ya sintofahamu inayoendelea klabuni hapo baada ya tetesi za kuondoka kwa kocha wao Pep Guardiola.
Kocha huyo mwenye uraia wa Uhispania, mkataba wake wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na kusema kuwa mustakabi wake atautoa katika siku za hivi karibuni huku tetesi zikieleza kuwa kuwa kuna uwezekano mkubwa kuondoka kwa kocha huyo huku nafasi yake ikitarajiwa kuchukuliwa na Muitaliano Carlo Ancelotti.
Muller amesema kwamba kuendelea kuwepo kwa hali hiyo hakuathiri kwa nmana yoyote utulivu wa wachezaji.
"Sisi hatujali kuhusu hilo," alisema Muller. "Tunataka kushinda kila kitu msimu huu, bila kujali nini kitajiri juu ya mustakabli wa kocha.
"Sifahamu kama atasaini mkataba mwingine mwishoni mwa msimu ama la, lakini endapo hatafanya hivyo pia hakuna tatizo. Jupp Heynckes pia alifanya hivyo mwaka 2012-13 na tulishinda makombe matatu msimu ule."

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video