MKUTANO Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliokuwa ufanyike mwishoni mwa wiki mjini Tanga, sasa hautakuwepo.
Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa TFF wametumiwa ujumbe mchana wa leo kutaarifiwa kwamba Mkutano huo hautakuwepo na sababu ni ukosefu wa fedha kufuatiwa kufungwa kwa akaunti zote za TFF kutokana na madeni ya kodi wanayodaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Mwishoni mwa mwezi uliopita, TRA ilizifunga akaunti zote za TFF kutokana na kukabiliwa na madeni ya kodi za mishahara ya makocha wa kigeni wa timu ya taifa, Taifa Stars, kuanzia wakati wa Marcio Maximo, Wadenmark Jan Poulsen, Kim Poulsen na Mholanzi Mart Nooij.
Hili linakuwa pigo la pili kwa TFF, baada ya awali kusitisha ziara ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment