Msimu wa majanga kwa kocha mwenye mbwembwe Jose Mourinho umeendelea kama kawaida!
Wakiwa ugenini usiku wa kuamkia leo, mabingwa watetezi wa ligi kuu England, Chelsea wamekubali kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya wenyeji Leicester City.

Magoli ya Leicester yalifungwa na Jamie Vardy dakika ya 38' na Riyad Mahrez dakika ya 48, huku Loic Remmy akiifungia Chelsea goli la kufutia machozi.
Ushindi huo umeifanya Leicester irejee kileleni mwa msimamo wa ligi kuu England ikijikusanyia pointi 35 ikiwa ni siku moja tu tangu Arsenal wakalie usukani kwa pointi zao 33.

Timu zote zimecheza mechi 16 na kocha wa Leicester, Claudie Ranieri ameendelea kuonesha kwamba amedhamiria kutisha msimu huu mzuri kwake na sasa yupo mbele kwa pointi 20 dhidi ya mabingwa hao watetezi.
Mourinho anashika nafasi ya 16 na ameshinda michezo minne tu msimu huu.
Mourinho anashika nafasi ya 16 na ameshinda michezo minne tu msimu huu.
0 comments:
Post a Comment