Saturday, September 26, 2015

Hatimaye Yanga leo wamevunja mwiko wa mahisimu wao Simba baada ya kuwashindilia mabao 2-0 katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu Tanzania bara uliopigwa kunako dimba la Taifa jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
Simba waliuanza mchezo huo kwa kasi na kutawala kwa umaridadi wa hali ya juu katika eneo la kiungo lakini kukosekana kwa umakini kwa washambuliaji wa Simba Mussa Hassan 'Mgosi' na Hamisi Kiiza 'Diego' kuliwafanya Simba kukosa fursa ya kupata bao.
Alikuwa ni mchezaji wa kimataifa wa Burudi ambaye pia aliwahi kuichezea Simba Amissi Tambwe alipoifungia Yanga bao la kuongoza mnamo dakika ya 44 baada ya kuungisha vizuri pasi aliyopewa na Mzimbabwe Donald Ngoma na kuamsha shamrashamra za mashabiki wa Yanga uwanjani hapo.
Mapaka mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0. Baada ya kurudi katika kipindi cha pili Yanga walianza mchezo huo kwa presha kubwa na ndipo mchezaji aliyetokea benchi Malimi Busungu kuunganisha kwa kichwa vizuri kabisa mpira uliorushwa na Mnyarwanda Mbuyu Twite na kuiandikia Yanga bao la pili mnamo dakika ya 79.
Simba waliajitahidi kupata walau bao la kufutia machozi lakini uimara wa safu ya ulinzi wa Yanga uliwanyima kabisa Simba kupata bao.
Yanga walipata pigo baada ta beki wao Mbuyu Twite kupewa kadi nyekundu baada ya kumtolea mwamuzi lugha chafu.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video