Friday, August 14, 2015

YANGA imeanza kuzua hofu kwa wapinzani wao katika kinyang’anyiro cha Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwamo Simba kutokana na mambo kadha wa kadha zaidi ikiwa ni ubora wa kikosi chao kilichosheheni wachezaji wengi wenye uwezo wa hali ya juu tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita.
Lakini pia kitendo cha timu hiyo kujichimbia jijini hapa, hasa katika eneo la Mbozi linalosifika kwa matukio kadhaa, kimeonekana kuwatisha wapinzani wao kwa kuamini si bure, lazima ‘Wanajangwani’ hao watakuwa na agenda ya siri.
Juu ya ubora wa wachezaji, Yanga inatajwa kama timu iliyokamilika kwa kiasi kikubwa kwani takribani kila nafasi ina wachezaji zaidi ya mmoja wote wakiwa na kiwango cha juu hivyo kuipa uwanja mpana wa kufanya vema kwasababu kila mchezaji atakayepewa nafasi atakuwa na uwezo wa kuibeba timu hiyo.
Miongoni mwa wachezaji wanaozipa tumbo joto timu kadhaa, zaidi ikiwa ni Simba, Azam na nyinginezo zenye nafasi ya kutwaa ubingwa msimu ujao, ni Geoffrey Mwashiuya aliyesajiliwa msimu huu akitokea Kimondo FC ya Daraja la Kwanza ambaye ameonyesha uwezo wa hali ya juu katika mechi mbalimbali za timu hiyo, ikiwamo michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika hivi karibuni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wengine ni Malimi Busungu aliyetokea Mgambo Shooting, Deus Kaseke (Mbeya City), Matheo Simon na Haji Mwinyi (KMKM), Donald Ngoma na Thaban Kamusoko (FC Platinum, Zimbabwe).
Chanzo:Bingwa

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video