MFUNGAJI Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, Simon Msuva, amewataka washambuliaji wenzake wa Yanga, akiwamo Mzimbabwe Donald Ngoma, kutotegemea mteremko kupata heshima ndani ya klabu hiyo, akiwasisitizia kupambana vilivyo.
Mbali ya Ngoma, Yanga imesajili straika wapya watano wengine wakiwa ni Deus Kaseke, Malimi Busungu, Geoff rey Mwashiuya na Matheo Simon ambao wanaungana na wale wa zamani kuunda safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Akizungumza na BINGWA kutoka Mbeya jana, Msuva alisema kuwa binafsi amejiandaa vizuri kuendeleza makali yake kama mfungaji na mchezaji bora wa msimu uliopita, akikiri kukabiliwa na ushindani mkubwa wa namba katika kikosi chao.
“Ni kweli kuna ushindani mkubwa wa namba lakini hilo si tatizo kwangu kwani inategemea na utendaji kazi wangu, nitaweka bidii ili niweze
kupata namba katika kikosi cha kwanza,” alisema.


0 comments:
Post a Comment