Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Akiwa na miaka 31 sasa nahodha wa zamani wa klabu za Yanga SC, Miembeni FC na Timu ya Taifa za Zanzibar na ile ya Muungano ‘ Taifa Stars’ Abdi Kassim ‘ Babi’ ameweka wazi kuwa hana mawazo ya kurejea kucheza soka nchini kwa wakati huu ligi kuu ya Malaysia ‘ Super Liga’ ikielekea Ukingoni.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu Ijumaa hii, Babi-Ballack wa Unguja ambaye ni nahodha wa Kikosi cha UITM FC iliyo nafasi ya nane katika ligi kuu ya Malaysia ameongeza kusema kuwa bado ana muda mrefu wa kucheza mpira wa Kimataifa ila ikitokea timu itayokubaliana naye nchini yuko tayari kurejea na kucheza.
“ Bado sijafikiria kurudi nyumbani , nina muda zaidi wa kucheza mpira wa Kimataifa . Baada ya Kutoka hapa naweza kujaribu Indonesia ama nitaendelea kubaki hapa Malasyia kwa kuwa kuna timu za ‘ Super League’ ambazo zinanihitaji. Ikiwa itatokea timu hapo nyumbani tukaelewana kimaslahi basi hakuna shaka nitarudi” anasema Abdi ambaye tayari amefunga mabao nane msimu huu, huku ligi ikiwa imesalia na michezo Mitano kwa kila timu.
Babi aliyewahi kuzichezea klabu za Mlandege ya Zanzibar, Mtibwa Sugar, Yanga SC, Azam FC, Dontam Lon ya Vietnam na sasa UITM FC amekuwa na uzoefu wa miaka zaidi ya kumi katika mpira wa ushindani. Ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa. Amekuwa akipewa unahodha na walimu mbalimbali katika klabu na timu za Taifa kutokana na namna anavyo wajibika, nidhamu yake pia iko juu kwa miaka yote.
0 comments:
Post a Comment