Zangale enzi za uhai wake
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salam za rambi rambi kwa Rais wa Chama cha Soka nchini Malawi (FAM), Walter Nyamilandu kufuatia kifo cha aliyekua Rais wa chama hicho John Zingale.
John Zangale alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi wiki iliyopita katika hospitali ya Mlambe iliyopo Blantyre nchini Malawi na kuzikwa mwishoni mwa wiki.
Zingale alikuwa Rais wa FAM mwaka 1998- 2002.
Katika salam zake kwenda kwa Rais wa FAM, Malinzi amewapa pole familia ya marehemu pamoja na chama cha soka nchini Malawi kwa msiba huo, na kusema TFF kwa niaba ya Watanzania iko pamoja nao katika kipindi hicho cha maombelzo.
0 comments:
Post a Comment