Mwishoni mwa juma lililopita Mayweather (kushoto) alitunukiwa tuzo ya Nevada Boxing Hall of Fame
Wakati huu akijiandaa kupanda ulingoni mwezi septemba mwaka huu dhidi ya Andre Berto, Floyd Mayweather aliomba ataje mabondia watano wakubwa zaidi kuwahi kutokea duniani.

Mayweather aliwashangaza watangazaji wa TV ya ESPN mjini Los Angeles baada ya kujitangaza mwenyewe kuwa ndiye bondia bora zaidi wa wakati wote.
Mr Money alijiita ni mtu wa ajabu zaidi kuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa masumbwi.

Mayweather alisema: "Nimewapiga mabingwa zaidi wa dunia kuliko bondia yeyote ndani ya muda mfupi. Nimewapiga wengi zaidi na nimepigwa kidogo sana".
0 comments:
Post a Comment