Mabingwa wa soka Afrika Mashariki na kati, Azam FC leo wanacheza mechi ya pili ya kirafiki uwanja wa Amaan Zanzibar ambapo wanakabiliana na Mafunzo ya visiwani humo.
Mechi hiyo ambayo inarushwa moja kwa moja na Chaneli mpya iliyozundiliwa jana ndani ya king'amuzi cha Azam TV, Azam Sports HD inaanza majira ya saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Mchezo wa kwanza katika dimba hilo, Azam walishinda 1-0 dhidi ya KMKM, bao pekee likifungwa na Gadiel Michael Mbaga aliyemalizia pasi ya Ramadhan Singano 'Messi'.
Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza kwa Messi kucheza tangu asajiliwe akiwa mchezaji huru baada ya TFF kuvunja mkataba wake na Simba.
Wanalambalamba wameweka kambi Zanzibar wakijiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga utakaopigwa Agosti 222 mwaka huu uwanja wa Taifa, Dar e saalam ukiashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu soka Tanzania bara itayoanza kutimua vumbi Septemba 12 mwaka huu .


0 comments:
Post a Comment