Waziri wa Utamaduni, Vijana na Michezo wa Suadan Mh. Stephen Lado Onesimo akizungumza na wachezaji wa Malakia FC
Waziriwa wa Utamaduni, Vijana na Michezo wa Sudani Kusini Mh. Stephen Lado Onesimo jana aliitembelea timu ya Malakia FC wakati ikifanya mazoezi kwenye uwanja wa Karume wakati ikijiandaa kwa ajili ya mchezo wake wa leo dhidi ya KCCA ya Uganda mchezo utakaopigwa majira ya saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Taifa ikiwa ni mwendelezo wa mashindano ya Kagame Cup hatua ya makundi.
Waziri huyo amesema, wachezi wa Malakia wanahitaji kushinda mchezo huo japo tayari wananafasi ya kucheza hatua ya robo fainali lakini ushindi kwenye mchezo huo utazidi kuwajengea heshima kwenye soka la ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati lakini pia watakuwa wanaweka heshima ya nchi yao (Sudan Kusini) ambayo imekuwa ikibezwa kwenye soka tangu ijitenge kutoka Sudan (Kaskazini).


“Nidhamu kwenye mchezo ni kitu muhimu sana, kila mtu anatakiwa awe na nidhamu ya hali ya juu wakati wa mchezo, muelekezane wenyewe kwa wenyewe muwapo uwanjani nani anatakiwa kufanya nini ili kumpunguzia kazi kocha wenu. Mimi nawatakia kila kheri na ninaimani na ninyi na ninamatumaini tutashinda mbele ya KCCA”, alimaliza.

0 comments:
Post a Comment