Manchester City jana imeichapa bao 1-0 klabu ya Melbourne katika mechi ya kirafiki ya maandalizi ya msimu mpya iliyopigwa mjini Melbiurne.
Goli pekee la ushindi lilifungwa na Samir Nasri dakika nne kabla ya mechi kumalizika.
Baada ya kusajiliwa kutokea Liverpool, Raheem Sterling hakucheza mechi hiyo, aliishia kuwaona wachezaji wenzake wa Man City akiwa jukwaani.
Lakini Sterling alionekana kwenye Screen kubwa za uwanjani na kujikuta akizomewa na mashabiki wa Liverpoool waliohudhuria mechi hiyo.
Tazama video ya Sterling kuzomewa:
0 comments:
Post a Comment