Thursday, July 30, 2015

Baada ya Azam FC kushinda mchezo wa robo fainali jana dhidi ya Yanga kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-3 na kufanikiwa kuungana na timu nyingine tatu ambazo tayari zilikuwa zimeshafuzu kucheza hatua hiyo. Azam inauna na Gor Mahia ya Kenya, Al Khartoum ya Sudan na KCCA ya Uganda kucheza nusu fainali ya michuano ya Kagame mwaka 2015.
Kitu ambacho kinavutia au siri ambayo watu wengi hawaijui kuhusu nusu fainali hizi mbili ni kwamba, timu zote zitakazokutana kwenye michezo ya nusu faili zimetoka kwenye kundi moja.
Azam ilipangwa Kundi C na timu za Adama City ya Ethiopia, Malakia ya Sudan Kusini pamoja na KCCA ya Uganda ambayo watakutana tena kwenye mchezo wa nusu fainali siku ya Ijumaa. Kwenye mchezo uliozikutanisha katika hatua ya makundi Azam iliibuka na ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na John Bocco ‘Adebayor’. Mchezo huo ulipigwa kwenye uwanja wa Taifa Jumapili Julai 19 siku moja baada ya ufunguzi wa mashindano hayo.
Hali kadhalika kwa Gor Mahia na Khartoum National Club ambazo zenyewe zimetoka pamoja kwenye kundi A lililokuwa na timu tano ambazo ni Yanga, Gor Mahia, KMKM, Teleco pamoja na Khartoum National Club.
Timu hizi zilikutana kwenye mchezo wa kundi A ambao ulipigwa siku ya Ijumaa Julai 24 na timu hizo kutoka sare ya kufungana goli 1-1 na sasa zitakutana tena kwenye mchezo wa nusu fainali.
Mechi hizi zinatarajiwa kuwa ngumu kwasababu kila mwalimu amepata kuona jinsi mpinzani wake anavyocheza, anatumia mfumo gani, wachezaji gani ni hatari na aina la soka linalotumiwa na mpinzani wake.
Khartoum ni timu ambayo haikuwa ikitajwa kufanya vizuri kwenye mashindano haya, lakini uzoefu wa muda mrefu na michuano mikubwa duniani wa kocha wa timu hii Kwesi Appiah umezidi kudhihirisha kuwa soka pia linahitaji makocha na wachezaji wenye uzoefu mbali na kuwa na kikosi kizuri kinachoundwa na wachezaji mahiri.
Kwesi Appia kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana alijiunga na Khartoum mwezi Disemba mwaka jana ameonekana kuwa na mbinu nyingi sana ambazo zimekuwa zikimpatia matokeo anayoyataka. Lakini pia anakutana na timu ngumu ya Gor Mahia ambayo inanolewa na kocha Frank Nuttal kikosi ambacho kimeshacheza mechi 18 nchini Kenya bila kupoteza na kikiwa hakijapoteza hata mchezo mmoja kwenye michuano ya Kagame.
Kwa upande wa Azam wao kikosi chao kinanolewa na kocha Stewart Hall ambae amebadilisha aina ya uchezaji wa Azam kwani kikosi hicho kwa siku za hivi karibuni kimekuwa kikicheza soka la pasi nyingi na kutengeneza mashambulizi kupitia pembeni, anakutana na timu ambayo inanolewa na kocha mzawa Mike Mutebi.
Mutebi anatambua vizuri kuwa walipokutana na Azam kwenye mechi yao ya kundi C alipoteza mchezo hivyo atakuwa makini kuzuia kufungwa tena kwa mara ya pili ndani ya mashindano yale yale.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video