Yanga SC wao kukipiga Jumatano
Michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi katika viwanja viwili vya Taifa na Karume vilivyopo jijini Dar es salaam, inaendelea leo kwa michezo miwili itayopigwa Uwanja wa Taifa.
Vinara wa kundi A timu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya, leo jumatatu watashuka dimbani kucheza na timu ya KMKM kutoka Visiwani Zanzibar.

Gor Mahia ambayo ilipata ushindi wa mabao 2- 1 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga, itakutana na KMKM ambayo iliibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya timu ya Telecom ya Djibout, mchezo utakaochezwa saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.
Mchezo wa kwanza utazikutanisha timu za Telecom ya Djibout dhidi ya Khartoum-3 kutoka nchini Sudan, ambayo itakua ikicheza mchezo wake wa kwanza.
Kesho Jumanne kutakuwa na michezo mitatu ambapo Al Shandy watacheza na LLB katika kundi B saa 8 mchana uwanja wa Taifa, Heegan FC dhidi ya APR uwanja wa Karume saa 10 jioni, Malakia dhidi ya Azam kundi C Uwanja wa Taifa saa 10 jioni.
Jumatano mabingwa mara tano wa michuano ya Cecafa Kagame Cup, timu ya Yanga SC watacheza dhidi ya Telecom ya Djibout saa 10 jioni uwanja wa Taifa, KCCA wakicheza na Adama City saa 10 jioni uwanja wa Karume, na Khartoum wakicheza mchezo wa awali saa 8 mchana uwanja wa Taifa dhidi ya KMKM.

Katika michezo iliyochezwa jana, Malakia ya Sudani Kusini iliibuka na ushindi wa mabao 2- 1 dhidi ya Adama City ya Ethiopia, LLB ya Burundi ikitoka sare ya bila kufungana na Heegan FC ya Somalia mchezo uliochezwa uwanja wa Karume, huku Azam FC wakiibuka na ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya KCCA ya Uganda.
0 comments:
Post a Comment