Radamel Falcao kwasasa anakula bata na familia yake nchini Marekani baada ya kukumbwa na msimu mgumu wa 2014-15 akiichezea klabu ya Manchester United kwa mkopo kutokea Monaco ya Ufaransa.
Falcao, 29, ambaye alichemshana timu ya Taifa ya Colombia mapema majira haya ya kiangazi katika fainali za Copa America nchini Chile, amepigwa picha akiwa na furaha kubwa katika fukwe za Miami, Florida, Marekani sambamba na mke wake, Lorelei Taron na watoto wao wa kike Dominique na Desiree.
Mapema mwezi huu, Straika huyo alijiunga na Chelsea kwa mkopo kutokea Monacho na sasa anajiandaa kupambana ili kudhihirisha ubora wake katika ligi ya England.

Falcao ameonekana mwenye furaha sana wakati huu akipunmzika na watoto wake Dominique na Desiree

Falcao anakula bata Marekani baada ya kukumbwa na wakati Mgumu Manchester United msimu wa 2014-15

Mtu na mke wanakula raha zao


0 comments:
Post a Comment