Wakati mashabiki wa soka wakisubiri kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu England Agosti 8 mwaka huu, tayari vituko vimeanza kutokea.
Shabiki mmoja wa kike wa Tottenham ame-share picha kwenye mitandao ya kijamii wikiendi hii akionesha Tattoo aliyochora sehemu ya tako yenye nembo ya Spurs.
Akiwa katika matembezi yake nje ya uwanja wa Arsenal wa Emirates, shabiki huyo wa Spurs alifunua nguo zake na kuonesha tako hadharani akiwa na lengo la kutamba na Tattoo yake kwa Wana Arsenal, ingawa mwanamke huyo alificha sura yake.
Msimu uliopita, Arsena walimaliza nafasi ya tatu na Tottenham walishika nafasi ya tano, lakini Spurs waliwachapa Gunners 2-1 White Hart Lane na wakatoka sare ya 1-1 Emirates.
Msimu ujao, Spurs watacheza na Arsenal Novemba 7 (Emiratse) na Machi 5 (White Hart Lane).
Tazama picha ya mwanake huyo hapa chini:

0 comments:
Post a Comment