leo ime-post jedwali moja linalovutia ambalo limejumlisha pointi zote za ligi kuu England walizokusanya kwa zaidi ya misimu 10 iliyopita.
Manchester United imekaa kileleni mwa jedwali hilo na shukuruni zimwendee Sir Alex Ferguson.
Hata hivyo Chelsea wapo nyuma kwa pointi moja tu.
Tangu kustaafu kwa Sir Alex Ferguson majira ya kiangazi mwaka 2013, Man United imekuwa na wakati mgumu katika michuano ya ligi kuu England na imemaliza nafasi mbili mbovu yaani nafasi ya 7 chini ya David Moyes na 4 ikiongozwa na Louis van Gaal.
Licha ya matokeo hayo, mashetani hao wekundu wameongoza jedwali hilo, huku Arsenal wakishika nafasi ya 3 na Liverpool 4.

0 comments:
Post a Comment