Thursday, June 11, 2015

Mshikemshike wa uchaguzi wa viongozi wa klabu ya Coastal Union tayari umeshaanza mara baada ya kamati ya uchaguzi ya TFF kufanya mchujo wa awali wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwenye klabu hiyo ya Wagosi wa Kaya ya jijini Tanga.
Wagombea watano wa nafasi ya ujumbe na mgombea mmoja wa nafasi ya uenyekiti wameondolewa katika kinyang’anyiro hicho baada ya kukosa sifa ya kuwa na elimu ya kidato cha nne kutokana na kutoambatanisha vyeti vyao vya elimu hiyo vinavyotambuli wa baraza la mitihani la taifa NECTA.
Hussein Abdul Ally aliyekuwa anagombea nafasi ya makamu mwenyekiti, ameondolewa kwasababu ya kukosa cheti cha elimu ya kidato cha nne. Wagombea wengine ambao wameondolewa kwa kukosa sifa hiyo ni pamoja na Hussein Ally Mwinyihewa, Omary Mwambashi, Mohamed Ally Mohamed maarufu kama ‘Dondo’ wakati Salumu Pelembe yeye hana uthibitisho wowote kwenye fomu zake hivyo kamati ya uchaguzi ya TFF kuamua kuliondoa jina lake.
Wagombea waliopitishwa kwa upande wa nafasi ya mwenyekiti ni Dkt. Ahmed Ally Twaha na mzee Steven Mguto ambaye pia alishawahi kupitishwa, lakini ametakiwa apeleke barua ya uthibitisho wa elimu yake kutoka baraza la mitihani la taifa NECTA.
Kwa upande wa makamu wa mwenyekiti, Salim Amir Fakki ndiye mgombea pekee aliyepitishwa kuwania nafasi hiyo baada ya wagombea wengine kuenguliwa kwasababu ya kutotimiza vigezo.
TFF itaanza kupokea mapingamizi yote kwenye ofisi zake jijini Dar es Salaam au wamkabidhi mjumbe wa kamati ya TFF kanda ya Tanga na Kilimanjaro Halid Abdallah ili aweze kuyatuma mapingamizi kupita baruapepe ya katibu mkuu wa TFF au ile ya TFF kabla ya Juni 13 mwaka huu. Juni 13 kamati ya uchaguzi itakuwepo jijini Tanga kupitia pingamizi kama zipo, Juni 14 itakuwa ni siku ya usahili kujua nani amepita na nani ameondolewa kabla ya kuelekea kwenye hatua ya uchaguzi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video