Shirika la utangazaji BBC limeripoti kuwa Mshambuliaji wa
Platinum FC ya Zimbabwe, Donaldo Ngoma anatarajiwa kuwasili Tanzania kwa ajili
ya kukamilisha mazungumzo ya kujiunga na mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga.
Mchezaji huyo
anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam muda wowote kuanzia sasa, kwa mujibu wa
uongozi wa Yanga.
Yanga, wakiwa na
kibarua cha kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika
mwakani, ipo katika mchakato wa kusajili wachezaji mahiri kwa ajili ya msimu
ujao wa 2015/16 wa ligi kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.
Yanga ilivutiwa na
Ngoma wakati ilipocheza na Platimun FC katika mechi za awali za Kombe la
Shirikisho mwaka huu na kuitoa timu hiyo kutoka kusini mwa Afrika.
0 comments:
Post a Comment