MENEJA wa Chelsea,Jose Mourinho amefungiwa kuendesha gari kwa miezi sita kaaba ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuzidisha mwendokasi alilolifanya mwaka jana.
Mwezi septemba 2014, Mreno huyo aliripotiwa kunaswa na Camera akiendesha kwa mwendokasi wa 60mph badala ya 50mph unaotakiwa katika ukanda A3 Esher bypass, mjini Surrey.
Kesi hiyo imesikilizwa jana katika mahakama ya Staines Magistrates na kocha huyo mwenye miaka 52 ameamuriwa kulipa faini ya paundi 910 kwa kuendesha kwa mwendokasi uliozidi 10pmh zaidi ya ule unaohitajika.
Pia anatakiwa kulipa faini ya paundi 750 na 75 ikiwa ni gharama za mahakama.
Hata hivyo, Mourinho hakuhudhuria mahakamani, lakini amekutwa na hatia baada ya kesi yake kusikilizwa.
Klabu ya Chelsea imekataa kutoa tamko baada ya kutafutwa kueleza hilo.
0 comments:
Post a Comment