Friday, June 12, 2015

Juma Nkamia

UMOJA wa timu za ligi daraja la kwanza Tanzania bara (FDL) kesho jumamosi unatarajia kufanya mkutano mkubwa na wa kihistoria jijini Dar es salaam kujadili changamoto mbalimbali za ligi hiyo na kutafuta namna ya kuzitatua au kuzipunguza.

Msemaji wa umajo huo, Masau Bwire amesema mgeni rasmi atakuwa naibu Waziri wa Wizara ya Habari, vijana, utamaduni na Michezo, Juma Nkamia atayeambatana na wageni waalikwa akiwemo Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, Dioniz Malinzi.

“Lengo kuu la mkutano huu ni kujaribu kuangalia changamoto zinazoikabili ligi daraja la kwanza na namna tunavyoweza kuzitatua au kupunguza. Pia ni kuangalia namna serikali na mamlaka za kusimamia mpira zinavyoweza kufanya ili kuboresha ligi daraja la kwanza” Amesema Masau Bwire na kuongeza: “Si tu kuboresha ligi daraja la kwanza, tuna mengi ya kuzungumza kuhusu soka la Tanzania. Ni mkutanao wa kihistora ambao wajumbe wa klabu zote 24 vinavyounda ligi daraja la kwanza wanakuja Dar kutoka kutoka mikoa mbalimbali na wataishi  kwa gharama zao”.


“Mgeni Rais atakuwa Naibu waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Juma Nkamia. Pia tumemualika mwenyekiti wa Baraza la michezo wa Taifa, Dioniz Malinzi na Rais wa TFF, Jamal Malinzi. Wote wamethibitisha kujumuika nasi katika mkutano huo”. Bwire amehitimisha.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video