Ngoma akisaini
Mshambuliaji nyota kutoka Zimbabwe, Donald Ngoma amesaini miaka miwili kuichezea Yanga.
Ngoma pamoja na kiungo Joseph Zuttah 'Tetteh' naye amesaini miaka miwili kuichezea Yanga.
| Tetteh akisaini Wote wawili jana walifanyiwa vipimo vya afya na kufuzu na leo wakafanya mazoezi na kikosi cha Yanga kabla ya kusaini mkataba leo. |
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, Isaac Chanji kwa kushirikiana na Katibu Mkuu, Dk Jonas Tiboroha ndiyo walishirikiana kukamilisha zoezi hilo.



0 comments:
Post a Comment