Bondia Floyd Mayweather una maneno mengi mno na ni vigumu
sana kumzuia asizungumze kitu hususani anapohudhuria matukio mbalimbali, lakini
nyota wa Pop Duniani, Rihanna ameweza kumziba mdomo bingwa huyo asiyepigika.
Jana usiku, imefanyika hafla ya kugawa  tuzo za Black Entertainment Television
Awards 2015 katika ukumbi wa  Microsoft
Theatre mjini California, Marekani, nyota wa R & B, Rihanna ameonekana  amekaa mezi moja na Mayweather, huku akishikilia
bandaji nyeusi.
Wakati hafla ikiendelea, Mayweather kama kawaida yake
akaanza kumwaga maneno, Rihanna akachukua ile bandeji na kumbandika nayo mdomoni
ili akae kimya, hakika watu waliokaa karibu yao wameonekana wakifurahia tukio
hilo. 

Rihanna akiziba mdomo wa  Mayweather

Mayweather anaonekana kutofurahia alivyofanyiwa na  Rihanna





0 comments:
Post a Comment