Dau la pauni milioni 35 lililotolewa na klabu ya Manchester United kwa ajili ya kumnasa beki wa kati wa Real Madrid Sergio Ramos limekataliwa na klabu ya mchezaji huyo. Madrid wamemwambia Ramos juu ya uamuzi huo baada mkurugenzi mkuu Jose Angel Sanchez kukutana na beki huyo kisiki walipokutana kwa ajili ya mazungumzo mafupi kwenye uwanja wao wa mazoezi Valdebebas.
Ramos, 29, ameondoka na kwenda kwenye mapumziko (likizo) huku amkiimbia klabu yake, anataka kufahamu mustakabali wa maisha yake ya baadae kabla timu hiyo haijaanza mazoezi ya kujifua kujiandaa na msimu ujao ‘preseason’ ambapo wachezaji wa klabu hiyo watakutana Julai 10 kwa ajili ya ziara ya Australia na China.
Ramos amesema anahisi hapewi thamani ndani ya Madrid ndio maana anataka kutimka ndani ya klabu hiyo lakini pia wachambuzi wa mambo wadai kuwa, Ramos anataka kutumi kigezo cha kutimkia Old Trafford ili kuipa presha Madrid ya kumpa mkataba mpya ambao utakuwa mnono.
Inafahamika Ramos anavuna mshahara kiasi cha pauni milioni 4 kwa mwaka akiwa Bernabeu na anataka aboreshewe mkataba ili awe anavuna kitita cha pauni milioni 6.5 kwa mwaka. Man U wao wamesema, wako tayari kumpa Ramos kitita cha pauni milioni 7.8 ikiwa kama mshahara wake kwa mwaka ili waweze kumnasa.
Manchester pia wanaelewa wanatakiwa kutenga dau kwa ajili ya kiungo wa Southampton Morgan Schneidrlin ili wamnase kiungo huyo.
0 comments:
Post a Comment