Nyota wa
klabu ya soka ya Barcelona, Muargentina
Lionel Messi aliachana na vyakula vya kisasa vya dukani ‘super market’ na
kuamua kutumia vyakula vya asili.
Daktari wa
mchezaji huyo bora mara nne wa dunia, Giuliano Poser amethibitisha kuwa ilibidi
kufanya mabadiliko ya chakula ili kumrudisha kwenye fomu yake ya zamani
mchezaji huyo.
Itakumbukwa
kuwa Lionel Messi alipoteza mara mbili mfululizo tuzo ya uchezaji bora wa dunia,
Ballon D’or kwa mpinzani wake wa muda
mrefu Cristiano Ronaldo baada ya kutokuwa na uwezo wake mzuri wa awali.
Pamoja na
klabu yake ya Barcelona kutofanya vizuri ndani ya misimu hiyo miwili mfululizo,
pia Messi alishindwa kuisaidia timu yake ya taifa ya Argentina ilipofungwa 1-0 dhidi
ya mabingwa wa sasa wa dunia Ujerumani kwenye mechi ya fainali ya kombe la
dunia la FIFA nchini Brazil mwaka jana.
Inaelezwa
kuwa baada ya kuanza vibaya msimu huu uliomalizika kwa Barcelona kushinda vikombe
vyote vitatu walivyoshiriki ‘treble’ Lionel Messi alimtafuta daktari huyo
Giuliano Poser ambaye aliwahi kumsadia mwaka 2008 alipokuwa na matatizo ya
kiafya.
Poser
anasema, “mara baada ya kombe la dunia, kila kitu kilibadilika kwa Messi” amezungumza
daktari huyo wakati akiongea na gazeti la Delo Sport la Hispania.
“Messi ni
kijana mpole na mtulivu. Hakuwa vizuri na akahisi kuna kitu kinahitaji
mabadiliko” Poser anaeleza
Barcelona
walianza kwa kususua msimu huu na hata kupelekea mikwaruzano baina ya wachezaji
na kocha wao Jose Enrique, lakini mambo yalibadilika ghafla na kushuhudia
wakirudi katika mstari na fomu ya Messi ikawa ndio chachu ya wao kumaliza na
vikombe vyote walivyoshiriki msimu huu.
“Alibadilisha
chakula, hatumii tena vyakula vya dukani. Anakula vyakula vyenye utajiri wa
vitamin, madini, mbogamboga na maziwa.” Anamalizia Poser daktari wa mchezaji
huyo.
0 comments:
Post a Comment