Kikosi cha England cha U21 kimeambulia kipigo cha nguvu kutoka kwa Italy kwenye mchezo wa kundi B kwenye michuano ya Mataifa ya Ulaya kwa vijana wenye umri wa miaka chini ya 21 (Ueropean Under 21 Championship) inayoendelea huko Jamhuri ya Czech.
Andrea Belloti alianza kuiandikia Italia goli la kwanza dakika ya 25 akimalizia kazi safi iliyofanywa na Domenico Berardi, dakika mbili baadae (dakika ya 27) Marco Benassi aliifungia Italia goli la pili na kuufanya mchezo kwenda mapumziko huku Italia ikiongoza kwa goli 2-0n mbele ya Uingereza.

Kichapo hicho kimeifanya Uingereza kutupwa nje ya michuano hiyo baada ya kumaliza mkiani mwa kundi B ikiwa na pointi tatu nyuma ya Italia yenye pointi nne, wakati Sweeden wao wako nafasi ya pili wakiwa na pointi nne huku Ureno ikiwa ni kinara wa kundi hilo ikiwa na pointi tano.
0 comments:
Post a Comment